[.:ENGLISH:.|.:ITALIAN:.|.:FRENCH:.|.:SWAHILLI:.|.:HINDI:.    
 
 


 

News letter subscription
   
Name
Email
 

 

 

 

 

 

 

 

 

BWANA HARUSI YUAJA

PDF  

Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya Bwana Harusi, tokeni mwende kumlaki.

-      Mathayo 25:6.

 

Je, waisikia sauti na kelele ya usiku wa manane? Na je, washuhudia kuingia kwa mabadiliko na muundo mpya ulio na kuelewana kwa Kiungu na upendo ambamo mna haki ya kweli iliyoimarika. Anayeridhi vitu vyote anadhihirika kwa hakika, na kwa kufunuliwa kwake mataifa na jamii zote duniani zaomboleza na zote zaja zikiwa zimetubu kwake. Mataifa na jamii zote duniani zafanyika zake Kristo, na Aonekana akitenda kupitia watu wa hali fulani duniani.

  Jua ya kwamba kuna jambo moja tu katika moyo wake Baba Aliye ndani mwetu kuwahusu wanadamu, na jambo hili ni lazima litatendeka na kukamilika katika wakati wake, na kila mwanadamu katika sehemu na daraja lake. Hili jambo pekee hata ingawa limedhihirishwa kwa njia na mifano mingi na miigo mingi sio linguine mbali ni kule kuja au kufunuliwa kwa (m)wana wake, wengine ambao wawezakuwa kwa sasa na kwa muda wamelala katika hali yao ya maisha ya kiwanadamu. Hili ndilo jambo ambalo lapaswa kusikika na kutamanika na kila mtu ambaye amapata kuuonja uhai ulio nje ya Ule Uzima uliofunuliwa kutoka mbinguni.  

Mapenzi ya kiungu yake Baba – kama mbegu iliyofichika ndani ya ardhi – ambayo ni maisha ya kiwanadamu, itachipuka, kuota maua, na kunawiri katika muda uliowekeka kiungu. Ilhali, kabla ya matawi kuchipuka kutoka ardhini wasio na darubini za imani hawataamini uhalali wa habari kama ile. Lakini kwa ghafula, kutoka upweke kwachipuka kile kilchokuwa kimefichika chini ardhini, kilichofichika kutoka kwanye macho yakikondoleacho ya wanadamu. Katika msimu huu, kwa kunusa kidogo kwa maji, mbegu iliyo ndani itachipuka na kuota kwa kunawiri. Kwako wewe unayefufuliwa leo na kwa majira haya, wahisi harufu ya maji haya?

 Hakuna amjuaye Mwana ila Baba, na hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na kama imefunuliwa kwako kutoka kwake Baba mbinguni. Hili lasalia kuwa siri iliyofichika hadi sasa, iliyofichika machoni mwa macho ya wanadamu wa siku hizi; na utukufu wao uko katika kutoa mihuri na kuleta ufahamu wa hii siri yake Baba na Mwana. Katika majira yaliyowekwa, kile kitabu kilichofungwa kwa mihuri katika nia za wale waliolala kwenye usingizi mkuu wa uwanadamu bila kufunguliwa na ile siri kuu kufunuliwa.  

Wakati siri hii inafunuliwa, Yule mwana huamka na Baba hudhihirika kwa uhakika kwa sababu mwanzo wake umesitirika na kupandwa katika Baba na kupitia ile kanuni ya kuzunguka, itamrudia Yeye Baba. Mwisho wa kiza hufanyika na hudhihirika kiuwazi kuwa Mwana Ndiye udhihirisho dhabiti wake Baba katika hii hali yetu ya unyonge wa mwanadamu.Wakati mwana anaukumbuka huo Mwanzo, yeye huanza kuutamani na kuuonea shauku huo Mwanzo; na huo Mwanzo hufanyika Mwisho.Kuugua kwake Yule mwana utakuwa: Baba, nitukuze na ule utukufu niliokuwa nao kabla ya kuumbika kwa huu ulimwengu. Si yasemekana kuwa wa kwanza ndiye mwisho, na wa mwisho ndiye kwanza? Ile hali ya mwisho basi ambayo yajulikana Mwaisho yapaswa kutamanika na kushaukiwa na kuonewa kiu kuliko jambo linguine lolote, kwa sababu katika hilo wapatikana Upumzisho wetu wa kweli na utukufu wetu.  

Pamoja na uamsho huo huja pia kufunuliwa kwa ile milki yake Mungu katika mbingu, ile nguvu, ule utukufu, ile furaha na amani isiyoelezeka. Mwanadamu  huvumbua kwa kweli kuwa kila kitu ni chake kwa uhakika, kwa utukufu wake na kwa kuvinjirika kwake. Katika majira yale, kila kanuni na dini yake mwanadamu kumhusu Mungu hupotelea na kuwa utupu, na Yule Atokaye Milele anaonekana kuwa Yote katika Yote. Naye Roho atadhibitisha katika yale majira wakati anasema, “katika ile siku mtajua kuwa Mimi Ndiye Aliye ndani yenu, nanyi ndani Yangu”. Hii ndio siku yake Bwana wakati mwanadamu hutambua kuwa yeye amefumwa akafumika kuwa mmoja naye Mungu; kuelewa huku ndiko Mwaisho.  

Mliolala, amkeni kutoka kwenye usingizi wenu na wingi wa utukufu wa mataifa yaliyo chini mwenu utafurika kama mito kwenu. Katika Nuru hii hakika, umasikini na uchi hufutiliwa milele kwa sababu Aliyevikwa na mavazi makuu ya Mfalme wa Utukufu amefunuliwa asifichike tena milele. Sikia kwa uhakika jogoo akiwika, ukasimame wima na ukashuhudie kucha kwa siku mpya – Siku Ya Bwana.  

Ile kelele, usiku wa manane ijulikanayo pia kama Tarumbeta ya Mwisho au Kelele ya Malaika Mkuu ni kelele ya uamsho kuingia katika uhakika wa mambo ambayo hayakutambulika mbeleni. Mambo ya Hakika ni kile kilichokuweko, kiko, na chasalia milele bila kupingwa na wakati; chasalia bila mawaa katika utukufu, na milele pia. Hii kelele kuu ya usiku wa manane ambayo hutokea kabla ya kucha kwa siku mpya na ya milele upande wa pili wa saa na wakati, itasikika na kila mtu alalaye katika wanadamu katika giza ya usiku wao. Katika kusikika kwayo ile sauti na kelele, tarumbeta zingine zozote huzimika, na sauti nyingi zingine kutoka kwenye mavumbi yaliyo chini ambayo humfunga mwanadamu kwenye hali ya kifo hutoweka, yasikawezesikika tena.  

Sikia Tarumbeta ya Mwisho ikilia na kwa uvumilivu ukakubali ikuongoze kuingia katika asubuhi ya siku mpya mahali ambapo vivuli na mafumbo huisha, ni Siku ya Milele ambayo Bwana pekee huishi ndani mwake. Wakati mafumbo yanafumbuliwa, na mitego kuteguliwa, na vivuli havimo tena, hapo basi utaelewa maneno yasemayo, “Mimi ndimi Bwana, na kando yangu hamna mwingine”. Rafiki, wezeni tulia katika maarifa haya, mkatiririke kama mito katika maarifa haya. Haya ni yako kuhifadhi milele. 

Waige wale mabikira watano wa lile fumbo ambao waliposikia kelele usiku wa manane iliyoashiria kuja kwake bwana harusi wanaamka kutoka kwenye uasi wa kulala kwao kwa wanadamu na kuingia katika utukufu wa ile harusi. Ujumbe unaoenezwa kutoka kwenye mdomo wake Bwana walia ukisema, “Amka, jiandae, na uje ukaungamanike na Bwana wako”.  

Amka, amka, jivike nguo zako, Ee Sayuni; jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi. Jikung’ute mavumbi; uondoke, Uketi, Ee Yerusalemu; Jifungulie vifungo vya shingo yako, Ee binti Sayuni uliyefungwa. (Isaya 52:1-2)  

Wanapoamka, kwa ghafla,, wanavumbua tena mavazi yao yang’aayo kwa weupe, ishara ya ubikira wao uliopotea kitambo walipolala kwenye kitanda cha upumbavu wa wanadamu. Wakati huu wote walikuwa bikira waliovikwa kwa mavazi ya nuru, lakini hawakuwezaona lile kwa sababu walikuwa katika giza, usingizi mkuu katika hali ya uongo ya wanadamu. Lakini hii hali ya uongo hubadilika wakati hawa bikira wenye hekima wenye mafuta salia wanapoamka na kuwasha taa zao. Papo hapo wanatambua hali yao kamilifu ya ubikira wao, ambayo yafaa kuposwa naye Mfalme. Muda tu wanapojitambua,  wanajikung’uta  kutoka kwenye mavumbi, ishara ya maisha ya kijinsia na kuketi kitawala na kipumziko. Ukiwezaamka katika kweli, kwanza utashtuka mwenyewe ukisema, “Kwani mwanadamu ni nani unamvisha taji la kifalme, na baadaye atawala juu ya vyote? “  

Hawa bikira wenye hekima wanafanyika hekima, sio kwamba wana tabia fulani za kidini, wenye miigo tamaduni ama wana cha kutoa dhabihu, lakini ni kuwa walikuwa wamejipatia mafuta kwenye vyombo vyao na kuweka taa zao zikiwaka katika ile siku ya kutembelewa kwao. Wakati wengine waitwao wajinga huketi tu wakijiingiza kwenye vitendo visivyo manufaa,  wale werevu hutafuta muda wa kutia jitihada kutafuta mafuta kutoka kwenye soko ambalo ni Roho.  

Kunalo soko ambamo hekima hulilia wanadamu waje na wanunue hekima bure bila pesa,na ile hekima yatoka juu kwake Baba wa Nuru, lakini mara kwa mara wanadamu huwa hawawezi kutambua huu mwito wanapozungukazunguka kujitafutia utukufu wao kwenye ulimwengu huu wa nje. Kama wangepata hii hekima kutoka kwa hili soko la Roho, wangetawala kwenye milki ya uzima.  

Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila dhamani. Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichisibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono. Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara. (Isaya 55:1-3)  

Katika kutafakari kwako na kuomba, unapobisha malango ya binguni, wewe hutafuta nini? Wewe huuliza nini? Kama wale mabikira wenye hekima, usiufuate unjia wa ule umatiwapendao usingizi wao katika ulimwengu ulio kiwiliwili cha ionekanayo kweli lakini batili na ambao hawawezikubali ufunuo wa Roho wakawezeona na kuikumbatia kweli ya kisichoonekana na macho ya kawaida. Uliza upako kutoka kwake Baba ambaye huwapa wote bila kupendelea wala kipimo. Tatuta yale mafuta kutoka juu ambayo yataiwasha taa yako na nuru ya uzima na kukusababisha wewe hatimaye kuridhi vilivyo kweli na vya milele.  

Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililichukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. (Yakobo 1:5-6)  

Mafuta ama upako ni ishara ya hekima ya kiroho na nuru kupitia Roho wa Mungu aliye ndani, amfanyaye mtu kuona kweli na mara tena kujulishwa kwa Nafsi yake isiyoonekana, isiyositirika, na imsababishayo kuukwepa ulimwengu huu utiao uharibifu na najisi. Hiyo nuru ya ile taa ya Bwana iliyo ndani, hufunua kisichoharibika, Aliye wa milele ndani, pamoja na bahari kuu ya utajiri wote wa kiroho ulio mikononi mwake yeye. Si ni ajabu kuwa upako ulio ndani ufunafunua utukufu na umbo la Mungu ambalo wewe ndilo? Huo upako hufungua fito za uongo na nia za kibinadamu ambazo humfunga mwanadamu Yule kwa hali maskini zinazoongozwa na kutawaliwa na hali ya ukawaida wa ulimwengu huu…majir na nyakati. Kutiwa nuru huku twaweza kukafikisha na kukuita kujitia nuru ambako kama hakuko, mwanadamu katika ukamilifu wake pekee aweza tu kuwa kitu dhoofu, kipofu, na kilicho uchi, na hicho ni kuonyesha haliya kuanguka kwake kupitia kile ambacho yeye hujifanyia malazi yake jehanamu. Wale mabikira watano wajinga hata ingawa walikuwa mabikira wasio mawaa wastahilio Bwana harusi, hawakuwezautambua ule ubikira wao wa kweli na utimilifu wao kwa sababu ya ujinga ulioko ndani mwao. Bila kijitia nuru ndani wanawezaje kuliona vazi lao linalong’aa, bila mawaa, hali ambayo ni ambatinifu na kuwa safi, bila dhambi, takatifu, na kamilifu mbele zake Mungu. Bila utakatifu, mwanadamu atawezaje kumwona Mungu, na kusimama mbele ya Patakatifu?  

Kama wale bikira watano wa lile fumbo, wengi wa siku tuliomo wasimama nje ya malango ya chumba chake bi harusi wakiitana na kuomba usiku na mchana, kusikia tu wakijibiwa tena na tena, "Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.” (Mathayo 25:12). 

Wanapogaagaa katika giza kule nje, wao hawaoni vile wanavyojulikana naye Mungu. Kwa sababu hawakubali upako ulio ndani mwao uwafunulie ukweli wa hali yao ya kiungu, ambayo Mwenye Enzi aliwaumba kwayo (ambayo ni Mungu); katika upumbavu wao wa kiwanadamu wanaunda mikakati ya kidini wakidhani hii itawafanya kuwa haki. Wanajitwika mizigo mizito ya kidini wakidhani hili litawafanya kufunguliwa mlango, bali wasikia yale maneno tena na tena, “Amin, nawaambia, siwajui ninyi.”  

Usikosee! Mungu humwona na kumtambua Yule Mwanadamu Mmoja toka Mwanzo, nah ii ndio njia pekee na lango la Utukufu. Hali ya mwanadamu wa kawaida na wa ulimwengu tulio, ambayo mwanadamu hujivika ni njia tu ya kuonyesha fikra ongo ambazo ni kama makombo ambayo ni lazima yafurushwe na kupeperushwa na kuwa tupu kupitia upepo wa ukweli. Mungu hakujui kama mtu wa ulimwengu na jinsia ya kinyama. Kama angekujua vile, ingemaanisha kuwa yeye hukubaliana na uongo.  

Pamoja na kujifunua kupitia upako ulio ndani, huja kuingia kupitia ule mlango wa kuingia kile chumba chake bi harusi na kuungamanika naye Bwana harusi. Huu mlango sio mwingine ila ni yale maarifa kutokuharibika, umilele, na Kweli tulio, ambayo haina mwanzo wala mwisho. Hii Kweli tulio ndiyo Mwanzo wa maumbile yake Mungu, Shahidi wa Kweli, Nyota ile ya Asubuhi, Mungu Mwenye Enzi. Kutambua na kukubaliana na Kweli hii iliyofichika chini ya ngozi ikufanyayo mwanadamu ndio mlango kuiingia ile Siku ya Bwana. "Mimi Ndimi mlango, Njia, Kweli na Uzima. Hakuna ajaye na kupaa katika Enzi na Milki hii ila kwangu Mimi"

Bikra walioamka na taa zao zikiwaka kwa ufunuo wa Kweli ile waingia katika chumba chake bi harusi kuungamanika naye Bwana harusi – Mfalme wa Milki ile – ambaye ni Kristo. Bi harusi ni wake Bwana harusi, naye Bwana harusi wake bi harusi. Wao ni Mmoja na hawatengeki milele. Haijaandikwa kuwa wale wawili watakuwa Mmoja? Haijaandikwa kuwa kuwa wale Bwana amewaunganisha pasiwe na kuwatenganisha? Hii yamaanisha, usikubali mawazo ya wanadamu – mwili na nyama, yanayojitambulisha kama mitungo na hekaya za kidini, yakutenge wewe kutokana na ukweli kwamba wewe ni Mmoja na Kristo – ufunuo na dhihirisho lake  

Mungu juu ya nchi. Kutoweka kwa hii hali ndio kifo, na jehanamu na dhiki kuu, na twajua kwamba Alifunuliwa ulimwenguni kukiharibu kifo; Naye hufanya vile kwa kuangamiza lile pazia kuwazalo kuwa liko, ambalo humtenganisha mwanadamu na Mungu wake.  

Bila kutambulika na wanadamu wa wakati huu tulio, uharibifu huu wa lile pazia unafanyika mara kwa mara katika harusi duniani kote wakati mikono ya bwana harusi inapofikia na kuondoa ile pazia-neti ifunikayo uso wake bi harusi na kumbusu yeye kwa ishara kuwa wameungamanika na kuwa mmoja.  Kuanzia pale, wao sio wawili tena bali ni mmoja. Kwa kweli siri zilizofichika zake Mungu zaonekana dhahiri kupitia mambo yanayoonekana duniani; Utukufu wake na maarifa yake yajaa ulimwengu kama maji yafunikavyo na kujaza bahari.  

Mwanadamu anapoendelea katika safari yake duniani, Roho aishiye wa Mungu daima anatafuta kumkumbusha na kumleta yeye mwanadamu katika ufahamu wa hali yake ya kuungamanika kwa kiungu na Muumba wake. Yale mawazo ya kiwanadamu na miigo ya kidini ipingayo kuungamanika huku kusikovunjika kati ya Mungu na mwanadamu, kwatokana katika mawazo duni ya kilimwengu ambayo milele yametenganika na zile siri za kiungu. Mawazo haya yatokana na hisia za kimwili za wanadamu. Na haya ndiyo yale mambo ya vilindi vya kishetani yanayochafua ulimwengu mzima, na kutia giza ufahamu wa wanadamu, na kwa hilo kuwafanya wapumbavu na wenye kupungukiwa na ukweli kuwa wao wamefunganika na kuwa mmoja na ule Utukufu wake Mungu. Katika wakati wa giza kuu la mwanadamu, yeye asimama nje ya malango yake bi harusi, asijue mlango uko wapi kwa sababu ya kutoelewa hali yake ya kweli na kamilifu kuwa yeye ni bikira katika umbo na mfano wake Mungu. 

Yeye hushindwa kujiona kuwa yeye ni bikira wa kweli, aliyevishwa mavazi yasiyo na mawaa, na aliyeposwa milele kwake Mfalme wa Utukufu. Ili akaweze tena patanishwa na uumbile ule wa kwanza zaidi ya ule mlango unaomweka nje, ambao kwa maneno mengine wajulikana kama Mbingu Mpya na Nchi Mpya ambayo Yesu kwa kufunuliwa kwake alimjulisha mwanadamu aliyeasi, inambidi aamke na ajinyenyekeze tena kwa muundo wa ndoa ya kweli toka mwanzo.  

Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii. Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe. (Marko 10:5-9)  

Hii ndio habari haswa ya ndoa na kuungamanika ambayo ilikabidhiwa kupitia torati na manabii kama mafumbo, lakini nia ya mwanadamu iliyo ngumu na isiyoamini, haiwezi kwa njia yoyote pata kupambanua kweli hii kuu. Kile Musa alichosikia Mlimani Sinai kilikuwa kishuhudie mwanzo wa uumbaji wa Mungu ambapo wale wawili (Mwanadamu na Mungu) ni mmoja; kumaanisha ufalme ambapo Mungu ni yote ndani ya yote. Torati ile ama sheria zile kumi zilikuwa ziufunue Mwili mmoja, Roho mmoja, Bwana mmoja, na Baba mmoja ambaye ni juu ya yote, kupitia yote na ndani yenu nyote. Huu ufunuo ukiingia ndani yako, wewe basi umepata mlango wa kupitia kurudi katika Baraka. Fikra za kijinsia za mwanadamu haziwezi kuupokea ukweli huu na kwa hivyo hupokea najisi na uongo kama vipande vya sheria kumi zilizovunjikavunjika. Musa kwa kuashiria alijitwika pazia juu ya uso wake kuonyesha vile nia ya mwanadamu isiyohisi hupokea uongo na najisi badala ya kweli iliyoko.  

Yesu angedhibitisha hili tena wakati anapokiri kuwa Sheria yote na Manabii waliposema ni: Sikia Ewe Israeli, Bwana Mungu wako ni Mmoja, utampenda Huyu Mmoja na moyo wako wote, nafsi yako yote, nia yako yote na nguvu zako zote. Na kanuni ya pili ni kama ile, kumpenda jirani yako kama ujipendavyo wewe mwenyewe. Kwa nini aseme, Sikia Ewe Israeli? Kwa sababu pasipokuwa na kuona kwa kweli kwa kiroho, yale maneno hayatakupa uhai. Watu wamejaribu kwa miaka na mikaka bila kufaulu kutii sheria zake Mungu kupitia maarifa yao wenyewe bila kujua siri ya ndoa.  

Wakati zile taa zang’aa na ukweli wa kibingu, hiyo huleta ufahamu wa kweli, na wakati ule ule, na kwa ghafula, mwanadamu huvumbua kuwa yeye ni mmoja kwa Roho na Mungu; hii ndio ile ndoa. Atajua kuwa katika hali yake ya kweli katika Bwana, na ataipenda nafsi yake kwa kweli kwa moyo wake wote, na nafsi, na nia, na nguvu zake zote. Na atona kwa kweli kuwa jirani yake ni Huyu Bwana Mwenyewe, kwa sababu kando yake hamna mwingine. Ni ndoa naye Bwana ambayo imekuwa toka milele na ambayo imeanza kurejeshwa sasa kwa neema. Sote tumeolewa naye Bwana, na Ufalme wake usioonekana, na mmoja kwa mwingine; sisi sote tunafanyika kuwa Yeye Aketiye juu ya yote.  

Katika ndoa hii, twaridhi jina mija, kichwa kimoja, uzima mmoja, utukufu mmoja; sisi ni wa Bwana na Bwana ni wetu. Bwana harusi aja; na aja kupitia na ndani yako unapoungamanika katika siri hii kuu ya Umoja Naye. Kwanza, wasikia ile kelele – Habari Njema, na baadaye waamka kutoka kwenye hali ya maisha ya wanadamu kuingia katika hali ya kumwelewa Bwana. Bwana wa utukufu – asiyeonekana hudhihirika na kuonekana ndani mwako, hii ndiyo siri ya uungu.  

Kama unyo masikio, jua kwa uhakika kuwa sasa ndio wakati; sikia kilio chake Bwana Harusi, uamke na uungamanike kwa umoja naye; amka ndani Yake. Ingia kupitia mlango ukaungamanike naye Bwana, ingia katika hali isiyoonekana, ingia katika Milele.  

Ubarikiwe.

Trevor Eghagha

trevor@sunrayministry.org

www.sunrayministry.org